Oktoba 10, 2019
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinaungana na Jumuiya ya Kimataifa na wapenda haki kote ulimwenguni katika maadhimisho ya 17 ya kupinga adhabu ya kifo. Siku hii huadhimishwa tarehe 10 ya mwezi Oktoba kila mwaka ikiwa na lengo la kuhamasisha kufutwa kwa adhabu ya kifo katika nchi zinazokumbatia adhabu hiyo.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ni mwanachama wa mtandao wa kupinga adhabu ya kifo duniani ‘’World Coalition Against Death Penalty’’ na tunaendelea kuelimisha umma juu ya madhara yanayoweza kutokana na adhabu hiyo sambamba na kuhamasisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kubadilisha adhabu hiyo kuwa adhabu ya kifungo cha Maisha. Kwa mujibu wa Ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania, 2018 jumla ya watu 480 wapo kwenye orodha ya watu waliohukumiwa adhabu ya kifo wakiwa gerezani kusubiri kunyongwa.
Ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, 1977 inalinda haki ya kuishi kwa kila mtu. Hata hivyo, ibara hii inaathiriwa na Sura ya 16 ya Sheria za Makosa ya Jinai zinazoweka adhabu ya kifo kwa kosa la uhaini, mauaji na ugaidi.
Pamoja na mtazamo chanya ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kauli aliyoitoa mwaka 2017 akiwa anamuapisha Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Hamisi Juma akieleza nia yake ya dhati ya kutokutia saini adhabu hiyo kwa ajili ya utekelezaji pamoja na kuwasamehe wafungwa 61 waliohukuwiwa kunyongwa katika sherehe za uhuru mwaka 2017; bado Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinasisitiza uwepo wa utayari wa kufutwa kwa adhabu hiyo katika sheria zetu na kuwa na adhabu ya kifungo cha maisha kama adhabu mbadala.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu tunapinga adhabu hii ya kikatili na inayotweza utu kwa sababu kuu zifuatazo:
Katika maadhimisho ya mwaka huu 2019, dhima kuu inaangazia namna ambavyo adhabu ya kifo huacha madhara kwa watoto na familia ambao wazazi/walezi wao wamehukumiwa adhabu ya kifo. Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kimeandaa Makala fupi ya video ikionesha simulizi ya wazee watatu kati ya watano ambao walihukumiwa kunyongwa kwa kosa la pamoja la mauaji, baadaye wakapunguziwa adhabu na kuwa adhabu ya kifungo cha Maisha na hatimaye wakaachiwa huru kwa msamaha wa Rais John Pombe Mgufuli. Kisa hiki kinaonesha namna ambavyo udhaifu wa mifumo ya utoaji haki unavyoweza kupelekea uonevu na jinsi ambavyo utekelezaji wa adhabu ya kifo unavyoweza kuwanyima washtakiwa nafasi ya kujitetea. Makala hii pia inaonesha namna ambavyo familia, hususani watoto, wanavyoathiriwa na kitendo cha wazazi au walezi kuhukumiwa adhabu ya kifo.
Kufuatia sababu hizi, Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kinatoa wito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuta adhabu hii katika sheria zinazoainisha kosa hilo na kuweka mbadala wa adhabu hiyo ikiwemo kifungo cha maisha au adhabu nyingine isiyohusisha kuua. Lengo la wito huu si kuwatetea wahalifu bali ni kupunguza madhara ya adhabu hii ya kikatili kwa jamii na kuendelea kulinda haki ya kuishi.
Imetolewa na;
Bi. Naemy Sillayo (Wakili)
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji
Unleash your inner purpose to help the helpless, marginalized and oppressed. Your contribution will help our course in provision of legal aid and promotion of human rights.
Help us curb human rights violations such as the murderous attack against people with albinism and elders.
Your donation will help us empower the general public with civic education on cross cutting issues counting gender issues and democracy to realize the changes we aspire.
Help us safeguard human rights all together.
Huenda huna muda wa kutosha wala kipato cha kutosha kulinda utu na haki za wengine, ingawa unawiwa kufanya hivyo.
Ni jukumu letu sote kujitoa kwa kidogo tulichojaaliwa ili kupaka rangi ya furaha katika nyuso za wengine, wewe, yule na sisi tukikusanya nguvu tunaweza kutetea na kulinda haki za wanaoonewa kwa kushindwa kuzifikia huduma za haki.
Jitolee sasa kidogo ulichonacho kusaidia ulinzi na utetezi wa haki na utu wa binadamu.

LEAVE A REPLY
Your email address will not be published.